Imarisha Mahusihano Yako na Mungu.

Utangulizi

Tangu mwanzo Mungu alijenga uhusiano mzuri na mwanadamu ( yaan Adamu ) sawa na Mwanzo 3:8-10;  “Kisha wakasikia sauti ya Bwana Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, Bwana Mungu asiwaone.Bwana Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi? Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha. Akasema, Ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! Umekula wewe matunda ya mti niliyokuagiza usiyale?”

Japokuwa mwanadamu alianguka, anguko lile halikuwa sababu ya Mungu kutokuonesha upendo wake kwa mwanadamu ( Mwanzo 3:21 “Bwana Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika.”

Hata baada ya hapo alimtuma mwokozi wa kumkomboa mwanadamu yule “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye.” Yohana 3:16-17.

Bado Mungu anahitajia mahusihano yetu na yeye ya imarike. Japokuwa yako mambo mengi yanayotuweka mbali na yeye, lakini bado nafasi ipo ya kutusogeza kwake, haijalishi tukoje, au historia yetu imekaaje bado sisi ni wathamani machoni pake.

Hapa chini ni baadhi ya mambo yatakayotusadia kuimarisha mahusihano yetu na Mungu wetu;

1.       Jitambue wewe ni nani kwa Mungu na Mungu ni nani kwako.

Mungu hupendezwa sana na mtu anayejitambua. Shetani humwogopa Sana mtu anayejitambua kutokujitambua ni moja ya silaha kuu anayoitumia adui shetani ili kutuweka mbali na Mungu. Yako maneno matatu yanayoweza kutusaidia katika kujitambua;

Ø  i. Mungu ni Baba yangu. (1  Yohana 5:18)

ii. Mimi Ni mtoto wake. ( Yohana 1:12 )

Kama tunavyofahamu kwamba baba hupenda Sana kuwa karibu na mwanae, na hupenda kumhudumia na hata pale mwanae anaposhusha kiwango chake cha mahusihano na babaye, baba hujitahidi sana kuyaongeza au kuyarudisha. Ndivyo ilivyo pia kwa Mungu

Ø  i. Mungu ni mfalme wa wafalme ( Ufunuo 19:11-19 )

      ii. Mimi Ni mwana wa Mfalme ( 1 Petro 2:9 )

Kama tunavyofahamu kwa habari ya Mfalme na Mwana wa Mfalme ( au uzao wa Kifalme ). Kwanza Mfalme huheshimiwa yeye na uzao wake wote. Sisi ni uzao wa Kifalme ( wa kiungu ). Tunapaswa kujitambua Hilo Kama vile Mungu anavyoheshimiwa katika dunia yote na sisi vivyo hivyo tunapaswa kupata heshima hii, lakini mara nyingi hujidharau na kujiona ni watu duni, wakati sivyo, sisi ni wathamani Sana!

Ø  i. Mungu ni Neno. ( Yohana 1:1; 1 Yohana 1:1 )

Ø  ii. Mimi napaswa kulitumia Neno la Mungu maishani ili lilete matokeo chanya. ( Yoshua 1:8 )

Kama Mungu ni Neno ni vizuri kuwa karibu na Neno lake ili tuweze kuwa karibu na Mungu, ili tuweze kuwa na mafanikio ya kiroho na kimwili na pia ustawi wa kiroho na kimwili. Hatupaswi kulidharau bali tulitumie  ili tufikie pale Mungu anapotaka tuwe au tuyafanye mapenzi yake.

2.       Kupenda kuwa karibu na Mungu.

Mungu hupenda kuwa karibu na sisi sana, pia huheshimu maamuzi yetu, kwa hiyo ni jambo la muhimu sana kupenda kuwa karibu naye kuliko kuwa mbali naye; dhambi, umasikini, ujana, ujane au kukosa malezi haviwezi kutuweka mbali na Mungu. Mungu ni baba yetu hutupenda sote, kwa hiyo anapenda uwepo wetu. Mtoto anayekaa karibu na mzazi wake hufaidi mengi hata Kama sio mali, hekima ya mzazi ni urithi tosha. Ndivyo ilivyo pia kwa Mungu wetu.

Haya ni baadhi ya mambo yatakayoweza kutusaidia kuongeza ukaribu wetu na Mungu.

i.                     Kuzungumza naye. ( Kwa njia ya maombi ).

Zamani za mababu, Mungu alizungumza nao kwa njia ya manabii na kwa njia mbalimbali, bali sasa anazungumza nasi kwa kupitia Mwanawe aliye Neno yaani Yesu Kristo, sawa na Waebrania 1:1 ndiyo maana unabii hupimwa kwa Neno.

Lakini haitoshi Mungu huzungumza nasi kwa Roho wake Mtakatifu. Tunaweza jiuliza Roho Mtakatifu anazungumzaje na sisi?

Kwanza tutambue ili Roho Mtakatifu azungumze na sisi inahitajika mahusihano ya karibu ya roho zetu na yeye.

Sasa tuone jinsi ambavyo Roho Mtakatifu hujihusisha na roho zetu.

·        Kuona huzuni rohoni ( Yohana 13:21)

·        Kukatazwa rohoni (Matendo 16:6-7)

·        Amani rohoni ( Wakolosai 3:15)

·        Kuzimia rohoni ( Matendo 22:17)

·        Msukumo rohoni ( Yeremia 20:9)

·        Kuchukizwa rohoni ( Matendo 17:16)

·        Kufadhaika rohoni (Yohana 13:21)

Hivyo sasa hii hutupa urahisi wa sisi kuzungumza na Mungu kupitia Roho wake Mtakatifu. Mtoto anapozidi kuzungumza na mzazi wake kila mara ndivyo anavyozidisha ukaribu wake na mzazi wake. Ndivyo ilivyo kwa Mungu wetu.

ii.                   Kumtumikia yeye

Mzazi hujisikia vizuri sana anapomwona mtoto anajishughulisha kwa ajili ya familia na watu wa nyumbani mwake. Vivyo hivyo na Mungu wetu yeye Kama mlezi wetu, na Baba yetu hupendezwa sana pale tunapofanya kazi ( huduma ) kwa ajili ya ufalme wake hapo ndipo humwaga baraka zake “Nanyi mtamtumikia Bwana, Mungu wenu, naye atakibarikia chakula chako, na maji yako; nami nitakuondolea ugonjwa kati yako.” Kutoka 23:25

iii.                 Kuwasaidia wahitaji.

Hii ni moja ya njia ya kuwa karibu na Mungu na ni Siri nzito iliyojificha kwao wasioamini, ila kwetu sisi tunaoamini na kulitambua  kusudi la Mungu, ndio tuliofunuliwa siri hii, Yesu  anasema atabagua kondoo na mbuzi. Mbuzi ni wale  ambao Yesu alikuja kwao ananjaa, lakini hawakumlisha; anakiu, lakini hawakumnywesha; yu uchi, lakini hawakumvisha; wata muuliza, Bwana ni lini ulikuja kwetu ukiwa uchi, lakini hatukukuvisha; ulikuwa mgonjwa hatukukutembelea. Naye atasema Kama mlivyowatendea mmoja wa hao walioko duniani mmenitendea Mimi. Ondokeni kwangu waovu ninyi nendeni motoni.

Lakini kondoo ni kinyume cha mbuzi hao atawaambia waingie katika raha yake wastarehe.

Hapa tunaona kuna makundi mawili kundi la mbuzi na kundi la kondoo. Kundi la mbuzi halikuwa na shutuma yoyote ya dhambi balo kosa lao ni moja tu, hawakukpenda kutoa misaada kwa wahitaji.

Tunapotoa kwa ajili ya wahitaji, tunamtolea Mungu naye hufurahi, na kiwango chetu cha kuwa karibu na Mungu huongezeka.

3.       Onesha upendo wako kwake.

Neno la Mungu linasema, hatuwezi kusema tunampenda Mungu lakini tunawachukia wenzetu, au ndugu zetu, tutahesabiwa kuwa sisi ni waongo. Hatuwezi kumpenda Mungu tusiyemwona kwa macho, huku tunawachukia ndugu zetu tunaowaona. (1 Yohana

Kwa hiyo upendo wetu kwa Mungu hupimwa kwa nje, kwa kuwapenda ndugu zetu.

Haya ni baadhi ya mambo yanayoonesha upendo wetu kwa Mungu;

i.                     Kujitoa

Kujitolea ni jambo la hiyari sana, mara nyingi watu hujitolea kufanya jambo au kumsaidia mwingine kwa moyo wa kupenda na wa huruma.

Kulingana na Neno la Mungu ambalo limekwisha kutangulia, ni kwamba huwezi kujitoa kwa ajili ya Mungu usiyemwona kama hauna tabia na moyo wa kujitolea kwa ajili ya watu wengine. Kinyume cha hapo sisi ni waongo.

Kujitoa ni sehemu ya kuimarisha uhusihano wa karibu na Mungu. Mungu huwabariki sana watu wenye tabia ya kujitolea kwa moyo wa kupenda.

ii.                   Kutoa tulivyonavyo kwa ajili yake.

Mungu huwabariki watu wanaotoa kwa ajili ya kazi yake na kwa ajili ya kueneza ufalme wake duniani.

Lakini hatuwezi kutoa kwa ajili ya huduma ya Mungu Kama hatuna tabia ya kujitoa kwa ajili ya wengine, tutaonekana waongo. Haiwezekani tukatoa kwa ajili ya Mungu wakati katikati yetu tunaowahitaji na tumewafumbia macho.

Kutoa ni sehemu ya kuimarisha uhusihano yetu na Mungu.

iii.                 Kumsifu na kumwabudu yeye.

Hakuna asiyependa kusifiwa hata na Mungu wetu hupenda kusifiwa. Tunapomsifu Mungu yeye hushuka katikati yetu na kutuhumia. ( Zaburi

Kusifu ni sehemu kubwa ya kuimarisha uhusihano yetu na Mungu ili ashuke tumtolee ibada.

Hitimisho

Mahusihano na Mungu ni hiyari yetu sisi wenyewe, Mungu yuko tayari kukaa karibu nasi. Kwa hiyo ndugu msomaji ni vyema tuzingatie hayo happy juu ili tuzidi kukua na kuongezeka katika kumjua yeye. Imeandaliwa

na kuandikwa na:

Mwalimu na Mwinjilisti:

Ebenezer Josephat Massawe.

WhatsApp na M-Pesa:

0748189017

Mungu akubariki Sana kwa kuendelea kusapoti Mafundisho haya.

IMARISHA MAHUSIHANO YAKO NA MUNGU.

Comments