Posts

Showing posts from June, 2021

Imarisha Mahusihano Yako na Mungu.

Utangulizi Tangu mwanzo Mungu alijenga uhusiano mzuri na mwanadamu ( yaan Adamu ) sawa na Mwanzo 3:8-10;   “Kisha wakasikia sauti ya Bwana Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga; Adamu na mkewe wakajificha kati ya miti ya bustani, Bwana Mungu asiwaone.Bwana Mungu akamwita Adamu, akamwambia, Uko wapi? Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi; nikajificha. Akasema, Ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! Umekula wewe matunda ya mti niliyokuagiza usiyale?” Japokuwa mwanadamu alianguka, anguko lile halikuwa sababu ya Mungu kutokuonesha upendo wake kwa mwanadamu ( Mwanzo 3:21 “Bwana Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika.” Hata baada ya hapo alimtuma mwokozi wa kumkomboa mwanadamu yule “Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.Maana Mungu hakumtuma Mwana ulimwenguni ili auhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe kati...